Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

JKCI Yakaribisha Wananchi Kupima Afya Bure
Jul 07, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_5920" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Profesa Mohamed Janabi akiteta jambo na baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi yake alipotembelea Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam leo. Kushoto ni Afisa Uhusiano wa Taasisi hiyo Bi. Anna Nkinda.[/caption]

Na: Frank Mvungi

 Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete imewataka Wananchi  kujitokeza kwa wingi kupima afya zao hasa magonjwa ya moyo katika msimu huu wa maonesho ya Kimataifa ya 41 ya Biashara ya Dar es Salaam yanayofanyika katika viwanja vya JK Nyerere jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika viwanja vya maonesho hayo Mkurugenzi Mkuu  wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi amesema kumekuwa na muitikio mkubwa sana kwa wananchi kutembelea banda lao ambapo amesema kuwa kwa siku takribani watu 700 wanafika katika banda hilo kwa ajili ya kupata huduma na ushauri.

[caption id="attachment_5923" align="aligncenter" width="750"] Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dkt. Bashir Nyangasa akielezea namna upasuaji wa moyo unavyofanywa kwa mmoja wa mwananchi aliyetembelea banda la taasisi hiyo katika Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) leo.[/caption] [caption id="attachment_5925" align="aligncenter" width="750"] Wananchi wakipata huduma ya vipimo katika banda la Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF) leo. (Picha na: Frank Shija)[/caption]

“Ni vizuri watanzania wakatumia fursa hii kufika hapa  na watapatiwa baadhi ya vipimo na ushauri  bure katika banda  letu lililopo ndani ya viwanja vya sabasaba kwa kuwa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuwahudumia wananchi wake kwa kuhakikisha kuwa wanapata huduma zote za msingi zenye kiwango na ubora,” Alisisitiza Prof. Janabi

Akifafanua  Prof. Janabi amesema  Taasisi hiyo imedhamiria kuwahudumia wananchi wakati wote wa maonesho na hata baada ya hapo wapo tayari kuwahudumia wale wanaohitaji huduma katika taasisi hiyo.

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete imekuwa ikitoa huduma za upasuaji wa moyo tangu kuanzishwa kwake hali inayosaidia kupunguza gharama zilizokuwa zinatumika kusafirisha wagonjwa kwenda nje ya nchi kwa matibabu kwa kipindi kirefu sasa.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi