Majaliwa Afungua Kongamano la Tano la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi
Oct 04, 2021
Na
Jacquiline Mrisho
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionesha kitabu cha Taarifa ya Utekelezaji wa Sera ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya Mwaka 2004 kwa Mwaka 2020/21 baada ya kukizindua katika Kongamano la Tano la Uwezeshaji Mwananchi Kiuchumi kwenye ukumbi wa Jengo la PSSSF Makole jijini Dodoma, Oktoba 5, 2021
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akibonyeza kitufe wakati alipozindua Kanzidata ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi baada ya kufungua Kongamano la Tano la Uwezeshaji Mwananchi Kiuchumi kwenye ukumbi wa Jengo la PSSSF Makole jijini Dodoma, Oktoba 5, 2021. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Geofrey Mwambe na kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Beng'i Issa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa pamoja na viongozi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja na wadhamini wa Kongamano la Tano la Uwezeshaji Mwananchi Kiuchumi baada ya kufungua kongamano hilo kwenye ukumbi wa Jengo la PSSSF Makole jijini Dodoma, Oktoba 5, 2021. Kulia kwake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji), Geofrey Mwambe