Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Magufuli Afungua Maonesho ya Biashara Sabasaba
Jul 01, 2017
Na Msemaji Mkuu

  • Awataka Wawekezaji Kutumia Fursa Zilizopo Nchini

 Na: Ismail Ngayonga

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewataka Mabalozi na Wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kutumia fursa za uwekezaji zilizopo nchini na kuisaidia miradi mikubwa ya kiuchumi ili iweze kuleta tija na maendeleo ya haraka kwa Watanzania.

Akifungua maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam leo, Rais Magufuli alisema Serikali ya Awamu ya tano itaendelea na dhamira yake ya kuhamasisha na kuimarisha mazingira ya uwekezaji ili kuhakikisha kuwa Watanzania wananufaika na rasilimali zilizopo ndani ya nchi yao.

[caption id="attachment_4970" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (katikati) akifuatilia sherehe za uzinduzi wa Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF) leo Jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yanafanyika katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere (Sabasaba) vilivyoko barabara ya Kilwa, kauli mbiu ya maonesho hayo ni “Ukuzaji wa Biashara kwa maendeleo ya Viwanda”. (Picha zote na: Frank Shija)[/caption]

Rais Magufuli alisema Serikali ya Awamu ya Tano imeendelea kushughulikia kero mbalimbali zilizokuwa zikiwakwaza wawekezaji ikiwemo utitiri wa kodi, ambapo katika bajeti ya mwaka 2017/18 Serikali imeondoa na kufuta kodi mbalimbali ili kuhakikisha kuwa dhamira ya ujenzi wa uchumi wa viwanda inafikiwa.

Aidha Rais Magufuli alisema katika kutimiza malengo ya uchumi wa Viwanda, Serikali imekusudia kufufua mradi  wa kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu za maji wa Stiegler’s Gorge wenye uwezo kuzalisha kiasi cha megawati 2100 za umeme, sambamba na kuongeza kiasi cha megawati 600 katika mradi wa kinyerezi III.

“Unapozungumzia Viwanda ni lazima uwe na umeme wa uhakika, hivyo Serikali ya Awamu ya Tano imechukua hatua muhimu kwa kufufua mradi wa  Stiegler’s Gorge kwa kutumia fedha zetu za ndani, kupitia mradi huu tutakuwa tumepata eneo la maji na kuhifadhi mazingira”  alisema Rais Magufuli.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Afri Tea Bw. Abdulkarim Mulla tuzo ya jumla ya wasambazaji bora wa bidhaa za ndani za vyakula nchini wakati wa sherehe za uzinduzi wa Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF) leo Jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yanafanyika katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere (Sabasaba) vilivyoko barabara ya Kilwa, kauli mbiu ya maonesho hayo ni “Ukuzaji wa Biashara kwa maendeleo ya Viwanda”. [caption id="attachment_4972" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia baadhi ya bidhaa za ngozi za zilizotengenezwa hapa nchini alizokabidhiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Mhandisi. Christopher Chiza mara baada ya kuzindua rasmi Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF) leo Jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yanafanyika katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere (Sabasaba) vilivyoko barabara ya Kilwa, kauli mbiu ya maonesho hayo ni “Ukuzaji wa Biashara kwa maendeleo ya Viwanda”.[/caption]

Aliongeza malengo ya Serikali ni kuwa na idadi kubwa zaidi ya viwanda vitakavyowezesha Watanzania kupata ajira, hivyo aliwataka Wafanyabiashara na Wawekezaji kutoka nje kutumia maonesho hayo kwa ajili ya kubaini fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo nchini.

Rais Magufuli pia aliwataka Wafanyabiashara hao kutumia fursa za maonesho hayo kwa ajili ya kubadilishana uzoefu katika maeneo ya teknolojia na kuimarisha ubia wa kibiashara miongoni mwao, na pia kutumia fursa ya kukutana na wateja kwa ajili ya kubaini mahitaji na mapungufu ya bidhaa zao.

[caption id="attachment_4975" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya washiriki wa Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaama maarufu kama sabasaba wakifuatilia hafla ya uzinduzi rasmi wa maonesho hayo leo Jijini Dar es Salaam. Kauli mbiu ya maonesho hayo mwaka huu ni “Ukuzaji wa Biashara kwa maendeleo ya Viwanda”.[/caption]

Kwa upande wake Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage alisema Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) na Wizara zimepanga kutumia fursa hiyo kwa ajili ya kuhamasisha Wawekezaji wanajitokeza katika ujenzi wa uchumi wa viwanda nchini.

“Katika maonesho haya kuna taasisi muhimu zinazohusika moja kwa moja katika suala zima la uwekezaji, TBS, SIDO, BRELA, TRA wapo katika maonesho haya kwa ajili ya masomo yanayohusu miongozo yote kuhusu fursa za uwekezaji zilizopo nchini” alisema Mwijage.

[caption id="attachment_4976" align="alignnone" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akichukua nembo yenye alama za bendera za mataifa ya Tanzania na Ujerumani alipotembelea banda la linalotumiwa na wafanyabiashara kutoka Ujerumani leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Balozi wa Ujerumani nchini John Reyels.[/caption]   [caption id="attachment_4969" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya TANTRADE, Mhandisi Christopher Chiza wakipunga mkono wakati wakimuaga Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF) leo. Maonesho hayo yanafanyika katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere (Sabasaba) vilivyoko barabara ya Kilwa, ambapo kauli mbiu ya maonesho hayo mwaka huu ni “Ukuzaji wa Biashara kwa maendeleo ya Viwanda”.[/caption]

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Mhandisi Christopher Chiza katika kuunga mkono na kuhamasisha kwa vitendo dhamira ya kufikia uchumi wa kati kupitia Viwanda ambapo kuanzia mwaka jana TanTrade imekuwa ikifanya maonesho ya viwanda kwa wajasiriamali mbalimbali.

Aliongeza kuwa malengo ya maonesho hayo ni kutoa fursa kwa Wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuweza kutumia fursa ya rasilimali mbalimbali zilizopo nchini zinaweza kutumia katika kuinua uchumi wa Watanzania.

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti huyo wa Bodi alitangaza kuongeza siku tano za maonesho ambapo sasa maonesho hayo yanatarajiwa kumalizika Julai 13 bada ya Julai 8 kama ilivyotangazwa awali.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi