Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Tathmini ya Mfanyakazi Aliyeumia Mahali pa Kazi Ifanyike Baada ya Mgonjwa Kupona- WCF
Sep 27, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_35744" align="aligncenter" width="750"] Washiriki na wakufunzi wa mafunzo ya tathmini za ulemavu unaotokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi yanayoendelea  mjini Singida chini ya uratibu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi - WCF.[/caption]

Tathmini ya ulemavu wa kudumu kwa mfanyakazi aliyeumia mahali pa kazi kuhakikisha kuwa mhusika amefikia kiwango cha juu cha kupona (Maximum Medical Improvement-MMI).

Hayo yamesemwa mjini Singida Septemba 25, 2018 na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omary kwenye mafunzo yanayoendelea ya  kuwajengea uwezo madaktari na watoa huduma ya afya ili waweze kufanya tathmini kwa mfanyakazi aliyeumia au kuugua kutokana na kazi kwa usahihi na Mfuko nutoe fidia stahiki.

“Kisheria kufanya assessment ya ulemavu wa kudumu ni baada ya mtu kufikisha MMI yaani Maximum Medical Improvement ikiwa ni kiwango cha juu cha kupona ambacho mfanyakazi aliyeumia yampasa kufikia na hapo ndipo daktari anaweza kufanya tathmini ya kiwango cha maumivu (madhara) aliyopata mfanyakazi huyo baada ya kuumia kutokana na kazi  ili hatimaye Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) uweze kutoa  mafao ya fidia stahiki.” Alifafanua Dkt. Omary.

Alisema, MMI ndiyo itamuongoza daktari kufanya tathmini assessment ya ulemavu wa kudumu kwa usahihi.

“Tarehe za MMI ni muhimu kwa Mfuko kwani ndio zitaamua (determine) kiwango anachostahili kulipwa mhusika” Alisema Mkurugenzi huyo.

Kumekuwepo na changamoto kwa baadhi ya Wafanyakazi walioumia, kuwashinikiza madaktari kufanya tathmini kabla ya wakati kwa kudhani mhusika ataweza kulipwa fidia, alisema Dkt. Omary

“Kwa mfano mfanyakazi aliyeumia na hajafikisha MMI asije kwako daktari kwakuwa anataka kwenda kulipwa fao la Fidia na kukushawishi umjazie fomu, na wewe unajaza zile fomu, unafanya impairment assessment, hii sio sawa na ni kinyume cha sheria.’ Alisema Dkt. Omary na kuongeza kuwa, tathmini (assessment) endapo haikufanywa kwa kuzingatia kanuni na miongozo, matokeo yake mhusika atarudi na kudai bado anaumwa na anahitaji kuendelea na matibabu.

Madaktari hao ambao wanatoka mikoa ya Kigoma, Tabora, Singida na Dodoma, wameanza mafunzo hayo Jumatatu Septemba 24, 2018 na mafunzo yatafikia kilele Septemba 28, 2018

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi