[caption id="attachment_35526" align="aligncenter" width="1000"] Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Protabas Katambi akiangalia maonesho ya picha wakati wa hafla ya Siku ya Amani Kimataifa iliyoadhimishwa kitaifa jijini Dodoma leo.Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni “Haki ya kuwa na Amani: Miaka 70 ya Azimio la Ulimwengu juu ya Haki za Binadamu.[/caption]
Na:Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma.
Viongozi wa dini nchini wametakiwa kutangaza amani ya nchi na kutotumia dini kugawa Wananchi ambapo inaweza kusababisha uvunjifu wa amani.
Hayo yameelezwa leo Jijini Dodoma na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Mhe. Patrobas Katambi alipokuwa akitoa hotuba wakati wa maadhimisho ya Siku ya Amani ya Kimataifa mwaka 2018 ambayo Kitaifa yamefanyika Jijini Dodoma.
[caption id="attachment_35527" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Protabas Katambi akizungumza wakati wa hafla ya maadhimisho ya Siku ya Amani Kimataifa leo Jijini Dodoma.Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni “Haki ya kuwa na Amani: Miaka 70 ya Azimio la Ulimwengu juu ya Haki za Binadamu.[/caption] [caption id="attachment_35528" align="aligncenter" width="1000"] Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Godfrey Mulisa akizungumza wakati wa hafla ya maadhimisho ya Siku ya Amani Kimataifa leo Jijini Dodoma.Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni “Haki ya kuwa na Amani: Miaka 70 ya Azimio la Ulimwengu juu ya Haki za Binadamu.[/caption]"Dini zote za Wakristo na Waislam zitangaze amani ya nchi. Dini zisitugawe kutokana na viongozi ambao sio wema, " alisema Mhe. Katambi.
Amesema, viongozi wa dini wana umuhimu mkubwa wa kulinda amani na haki za binadamu, ambapo Watanzania wameendelea kulinda amani hiyo pamoja na haki za binadamu.
Aidha amesema, ipo mifano mingi ya uvunjifu wa amani katika nchi za jirani na za mbali ambapo kumesababisha vifo, ulemavu na uhalibifu mkubwa wa miundombinu.
[caption id="attachment_35529" align="aligncenter" width="1000"] Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo akizungumza wakati wa hafla ya maadhimisho ya Siku ya Amani Kimataifa leo Jijini Dodoma.Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni “Haki ya kuwa na Amani: Miaka 70 ya Azimio la Ulimwengu juu ya Haki za Binadamu.[/caption] [caption id="attachment_35530" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya washiriki wa maadhimisho ya Siku ya Amani Kimataifa 2018 wakifuatilia mada katika hafla ya ufunguzi wa maadhimisho hay oleo Jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_35531" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Protabas Katambi akijadiliana jambo na Wakili Mkuu wa Serikali, Clemence Mashamba(kulia) na Mkurugenzi wa Jinsia toka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Julius Mbilinyi.[/caption] [caption id="attachment_35532" align="aligncenter" width="1000"] Wakili Mkuu wa Serikali Clemence Mashamba akifafanua jambo wakati wa mjadala kuhusu Haki za Binadamu na dhana ya Utawala Bora katika maadhimisho ya Siku ya Amani ya Kimataifa leo Jijini Dodoma. Kutoka kulia ni Mwendesha mjadala Ernest Sungura na Mkurugenzi wa Tume ya Utawala Bora na Haki za Binadamu, Bibi. Mary Massey.[/caption] [caption id="attachment_35533" align="aligncenter" width="1000"] Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Protabas Katambi(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na watoa mada mara baada ya kufungua kongamano maalum kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Amani ya Kimataifa iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa(UN) leo jijini Dodoma .(Picha zote na: Idara ya Habari –MAELEZO)[/caption]Hivyo amewataka Watanzania kushikilia amani waliyonayo kwani ndio tunu pekee waliopewa na Mungu na kwa pamoja walinde haki na amani ya nchi.
Vilevile amewataka waandishi wa habari kutumia vyema kalamu zao pamoja na Wanasiasa kutumia ndimi zao vizuri na kuacha siasa za uchochezi ili kulinda amani ya nchi.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa UNDP Godfrey Munisi amesema Tanzania ni nchi isiyo na machafuko na UNDP itaendelea kuhakikisha Tanzania inaendelea kudumisha amani iliyonayo.
Kauli mbiu ya mwaka huu ya maadhimisho hayo ni Haki ya Kuwa na Amani: Miaka 70 ya Azimio la Ulimwengu Juu ya Haki za Binadamu