[caption id="attachment_35516" align="aligncenter" width="900"] Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazia akitoa taarifa rasmi ya Serikali kuhusu ajali ya kivuko cha MV Nyerere kilichokuwa kikisafiri kutoka Bugorora kuelekeaKisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe mkoani Mwanza jana.[/caption]
Na: Mwandishi Wetu - MAELEZO
Bendera ya Taifa kupandishwa nusu mlingoti kwa muda wa siku tatu kufuatia ajali mbaya ya Kivuko cha MV Nyerere iliyotokea jana wakati ikifanya safari yake kati ya Bugorora na Kisiwa cha Ukara Wilayani Ukerewe mkoani Mwanza.
Akitoa taarifa hiyo leo jijini Dodoma Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi amesema kuwa Serikali inatoa pole kwa wanafamilia wote walioguswa na ajali hiyo na kuongeza kuwa Serikali imeendelea na zoezi la ukoaji kwa kushirikiana na mamlaka zingine.
[caption id="attachment_35517" align="aligncenter" width="1000"] Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazia akitoa taarifa rasmi ya Serikali kuhusu ajali ya kivuko cha MV Nyerere kilichokuwa kikisafiri kutoka Bugorora kuelekeaKisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe mkoani Mwanza jana. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge), Maimuna Tarishi na Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Bibi. Rehema Madenge.[/caption]"Kutokana na kuombeleza msiba huu mkubwa kwa Taifa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametangaza maombolezo na kuagiza Bendera ya Taifa kupeperushwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzi kesho tarehe 22 -24 Septemba "alisema Balozi Kijazi.
Katika hatua nyingine Balozi Kijazi amesema kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba ajali hiyo inawezekana kuwa imesababishwa na kubeba abiri zaidi ya kiwango chake, Serikali imeagiza kukamatwa kwa wale wote wanaohusika na uendeshaji wa moja kwa moja wahojiwe, na wale wote watakaobainika kuhusika kwa namna moja ama nyingi watachukuliwa hatua zaidi.
[caption id="attachment_35519" align="aligncenter" width="1000"] Baadhi ya Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa wakimsikiliza Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi alipokuwa akitoa taarifa rasmi ya Serikali kuhusu ajali ajali ya kivuko cha MV Nyerere kilichokuwa kikisafiri kutoka Bugorora kuelekeaKisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe mkoani Mwanza jana. (Picha na Idara ya Habari - MAELEZO)[/caption]Aliongeza kuwa wale wote wanaohusika katika uendeshaji wa Kivuko hicho wahojiwe ili kubaini ukweli na hatua stahiki ziwezekuchukuliwa huku na kuongeza kuwa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA), kwa kuwa ndiyo chombo kinachofanya ukaguzi wa vyombo vya usafiri wa majini.
Katika taarifa hiyo aliyoisoma leo jioni jijini Dodoma wakati kihitimisha Kiko Kazi cha Makatibu Wakuu, M,anaibu Katibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa balozi Kijazi amesema kuwa hadi kufika leo saa 9:10 mchana watu 47 walikuwa wameokolewa wakiwa hai huku 127 wakiwa wamefariki.