Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Uchukuzi na Mawasiliano) Mhandisi Atashasta Nditiye (wa tatu kulia) akiwa meza kuu pamoja na baadhi ya wawakilishi wa Umoja wa Posta kwa nchi za Kusini mwa Afrika (SAPOA), katika mkutano wa umoja huo, alioufungua leo, ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwan'gombe na wa pili ni Mwenyekiti wa Bodi ya TPC, Kanali Mstaafu, Dk. Haruni Kondo. Baadhi ya wawakilishi kutoka DHL ambao ni wafadhili wa mkutano huo wakifuatilia maelezo mbalimbali kutoka kwa wawakilishi wa nchi mbalimbali za umoja huo. Wawakilishi kutoka Shirika la Posta Tanzania (TPC) wakiskiliza kwa makini maelezo mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa na wawakilishi wa nchi za umoja huo, wakati wa ufunguzi wa mkutano huo. Kutoka kushoto ni Kaimu Meneja Uendeshaji wa Biashara, Mwanaisha Saidi, Kaimu Meneja Rasilimali za Shirika, Macrice Mbodo na Meneja Huduma za Fedha, Rehema Mbunda. Baadhi ya wawakilishi kutoka nchi za Kusini mwa Afrika zilizounda umoja huo, wakifuatilia kwa makini hotuba na maelezo mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa katika mkutano huo. Baadhi ya wawakilishi wa umoja wa SAPOA, kutoka nchi za Kusini mwa Afrika, wakifuatilia kwa makini mkutano huo. Mtendaji Mkuu wa Posta wa Mauritius, Giandev Moteea, akitoa hotuba yake katika mkutanoni huo.