Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Matukio Katika Picha Uzinduzi wa Matokeo ya Utafiti wa Kilimo na Mifugo 2016/17
May 16, 2018
Na Msemaji Mkuu

Waziri wa Mifugo na Uvuvi  Mhe. Luhaga Mpina  akisisitiza umuhimu wa kutumia takwimu na Tafiti  mbalimbali katika kuchochea maendeleo na kufanya maamuzi mbalimbali kabla ya kuzindua matokeo ya utafiti wa Kilimo na Mifugo wa mwaka 2016/2017 katika ukumbi wa Ofisi za Taifa za Takwimu (NBS) leo Jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akitoa maelezo ya awali kuhusu matokeo ya utafiti wa Kilimo na Mifugo wa mwaka 2016/2017 katika ukumbi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) leo Jijini Dodoma.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi  Mhe. Luhaga Mpina  akikata utepe kuzindua  matokeo ya utafiti wa Kilimo na Mifugo wa mwaka 2016/2017 katika ukumbi wa Ofisi  ya Taifa ya Takwimu (NBS) leo Jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Programu za Kimataifa  wa Shirika la USADA-NASS  Bw. Mark Miller akizungumza wakati wa  uzinduzi  ripoti ya matokeo ya utafiti wa Kilimo na Mifugo wa mwaka 2016/2017 katika ukumbi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) leo Jijini Dodoma.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi  Mhe. Luhaga Mpina  akimkabidhi   Muwakilishi wa Benki ya Dunia hapa nchini Bi Elizabeth Ann Talbert  ripoti ya matokeo ya utafiti wa Kilimo na Mifugo wa mwaka 2016/2017 katika ukumbi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) leo Jijini Dodoma.

Sehemu ya wageni walioshiriki hafla ya uzinduzi  matokeo ya utafiti wa Kilimo na Mifugo wa mwaka 2016/2017  wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi  (hayupo pichani) katika ukumbi wa Ofisi za Taifa za Takwimu (NBS) leo Jijini Dodoma.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi  Mhe. Luhaga Mpina  akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa hafla ya kuzindua  matokeo ya utafiti wa kilimo na mifugo wa mwaka 2016/2017 katika ukumbi wa Ofisi  ya Taifa za Takwimu (NBS) leo Jijini Dodoma.

                                                                      (Picha zote na Frank Mvungi )

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi