Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Magufuli Awatunuku Kamisheni Maafisa Wapya 197 wa Jeshi
Feb 03, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_28443" align="aligncenter" width="750"] Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride la Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi pamoja na baadhi kutoka nchi marafiki kabla ya kuwatunuku Kamisheni katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam (Picha na Ismail Ngayonga - MAELEZO).[/caption]

Na. Fatm Salum

Rais John Pombe Magufuli amewatunuku kamisheni Maafisa wapya 197 wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika sherehe zilizofanyika leo ikulu jijini Dar es Salaam.

Maafisa hao wapya wa Jeshi kundi la 62 la mwaka 2017, wamehitimu mafunzo ya kijeshi katika Chuo cha Mafunzo ya Jeshi Monduli kilichopo mkoani Arusha.

[caption id="attachment_28442" align="aligncenter" width="750"] Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwatunuku Kamisheni Maafisa wapya 192 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania pamoja na Maafisa kadhaa kutoka nchi marafiki katika Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.[/caption]

Maafisa waliotunikiwa kamisheni wanaume ni 169 na wanawake 28 wakiwemo Maafisa wageni 14 waliotoka nchi za jirani na nchi rafiki na Tanzania.

Aidha katika sherehe hizo Rais Magufuli alikagua gwaride na kutoa zawadi kwa Maafisa waliofaulu vizuri zaidi kwenye kozi mbalimbali wakati wa mafunzo yao.

[caption id="attachment_28444" align="aligncenter" width="750"] Mafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi wakivalishana vyeo mara baada ya Kutunukiwa Kamisheni na Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.[/caption]

Chuo cha Mafunzo ya Jeshi Monduli kilianzishwa mwaka 1969 na Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere eneo la Kurasini Jijini Dar es salaam na mwaka 1976 kilihamishiwa wilayani Monduli mkoani Arusha.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi