Na. Immaculate Makilika- MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amempongeza na kumshukuru Rais wa Uganda, Yoweri Museveni kwa kuwa miongoni mwa viongozi wanaoendeleza fikra za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, ikiwa ni kielelezo cha kuendeleza uhusiano mzuri ulipo baina ya nchi mbili za Tanzania na Uganda.
Akizungumza leo Ikulu jijini Dar es salaam, akiwa pamoja na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, aliyewasili nchini kwa ziara y...