Wazri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu waongeze kasi ili utendaji kazi Serikalini uweze kufikia hatua nzuri.
“Ninawashukuru watumishi wote kwa ushirikiano mnaotupatia mimi pamoja na mawaziri wenzangu, makatibu wakuu wote watatu, wakurugenzi mbalimbali na wakuu wa vitengo. Tunatakiwa tuongeze kasi ili tufikie hatua nzuri ya utendaji kazi Serikalini,” alisema.
Alitoa kauli hiyo jana usiku (Jumanne, Mei 28, 2019) alipokutana na viongozi na watumishi wa ofisi yake na kufuturu nao pamoja kwenye makazi yake jijini Do...
Read More