Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Geji ambapo alipata fursa ya kusikiliza changamoto mbalimbali za wananchi wa maeneo ya Shehia ya Kijichi, wilaya ya Magharibi A, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja ambapo awali kabla ya mkutano huo alipata fursa ya kufanya Kikao cha Ndani na Uongozi wa Jeshi la Polisi Visiwani Zanzibar. Kushoto ni Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamad Khamis Hamad na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Magharibi A, Suzan Kunambi.
Read More