WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Viongozi wa Serikali wasiokuwa na mashamba ya mikorosho kutojihusisha na biashara ya uuzaji wa zao hilo.
“Kama huna shamba, huwezi kuwa na korosho, unauza umepata wapi. Jukumu lenu ni kufuatilia, kukemea na kuchukua hatua stahiki penye udhaifu na si vinginevyo.”
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Septemba 17, 2017), wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa korosho uliofanyika mkoani Tanga.
Amesema kama viongozi hao wanahitaji kuuza korosho watumie muda huu ambao Serikali inahamasisha watu wafu...
Read More