[caption id="attachment_14113" align="aligncenter" width="944"] 5. Balozi Dkt. Nchimbi akiendelea na mazungumzo na ujumbe wa Serikali ya Brazil (Hawapo pichani)[/caption]
Na: Mwandishi Wetu
Serikali ya Brazil imesamehe Tanzania deni la jumla ya Dola za Marekani milioni 203 ambazo ni sawa na shilingi za Kitanzania zaidi ya Bilioni 445. Deni hilo lilitokana na mkopo uliotolewa kwaajili ya ujenzi wa barabara ya Morogoro-Dodoma mwaka 1979 pamoja Riba.
Balozi wa Tanzania Nchini Brazil Dkt. Emmanuel Nchimbi alisaini mkataba huo kwaniaba ya Tanzania huku Wakili wa Hazina ya Taifa Dkt. Sonia Portella Nunes akisaini kwa niaba ya Serikali ya Brazil.
[caption id="attachment_14116" align="aligncenter" width="944"] Balozi Dkt. Emmanuel J. Nchimbi akisaini kwa niaba ya Serikali ya Jamnhuri ya Muungano wa Tanzania Mkataba kuhusu Msamaha wa Deni la Tanzania kwa Serikali ya Brazil. Kwa upande wa Brazil mkataba huo ulisainiwa na Dkt. Sonia Nunes, Wakili wa Serikali ya Brazil.[/caption] [caption id="attachment_14119" align="aligncenter" width="944"] Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akibadilishana mkabataba huo na Dkt. Sonia Nunes, Wakili wa Serikali ya Brazil mara baada ya kusaini mkataba wa msamaha wa deni.[/caption]Balozi Nchimbi alishukuru Serikali ya Brazil kwa Msamaha huo ambao alisema umeunga mkono jitihada za Rais Dkt. John Pombe Magufuli kujenga uchumi imara wa Tanzania.
Balozi Nchimbi pia aliihakikishia Serikali ya Brazil utayari wa Tanzania katika kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na uchumi na Brazil.
[caption id="attachment_14122" align="aligncenter" width="944"] BaloziDkt. Emmanuel Nchimbi akiongoza ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo na Serikali ya Brazil.[/caption] [caption id="attachment_14125" align="aligncenter" width="944"] Balozi Dkt. Emmanuel J.Nchimbi pamoja na Mkuu wa Ujumbe wa Serikali ya Brazil Bw.Guilheme Laux (kulia kwa Balozi Nchimbi) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wapande zote mbili[/caption]Kiongozi wa ujumbe wa Brazil kwenye sherehe hiyo Bw. Guilheme Laux, Undersecretary of Credit and Guarantee kutoka Wizara ya Fedha ya Brazil alimtamka rasmi kufunguliwa kwa milango ya ushirikiano wa kifedha na kibiashara iliyokuwa imefungwa kutokana na Deni hilo lililofanya Tanzania kuwa moja ya nchi zenye madeni sugu ya Brazil.
Hivyo kutoka sasa Makampuni ya Brazil yanaruhusiwa kukopa katika Benki za Brazil kwa ajili ya kutekeleza miradi nchini Tanzania lakini pia Serikali ya Tanzania inaruhusiwa kuanzisha majadiliano ya miradi mipya ya maendeleo.