TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea msaada wa magari matatu yenye thamani ya Dola za Marekani 99,700 kutoka Kampuni ya Foton International Trade Co. Ltd ya nchini China.
Amepokea msaada huo leo (Jumatano, Agosti 9, 2017) jijini Dar es Salaam, ambapo amesema magari hayo yatatumika katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya jamii nchini. Magari hayo ni Sauvana SUV moja na Tunland Double cabin mbili.
“Nashukuru kwa msaada huu wa magari uliotolewa na Kampuni ya Foton kwa Serikali yetu. Magari haya yanaweza kutumika...
Read More