Mafundi wakiendelea na ujenzi wa kivuko kipya cha Ijinga Kahangala kinachojengwa katika karakana ya Songoro Marine iliyoko Ilemela mkoani Mwanza, kivuko hicho ambacho ujenzi wake unagharimu shilingi bilioni 5.2, kitakapokamilika kitakuwa kikitoa huduma kati ya Ijinga na Kahangala wilayani Magu mkoani Mwanza, kitakuwa na uwezo wa kubeba abiria 200 na magari 10 sawa na tani 100. Ujenzi wa kivuko hicho na vingine vipya na ukarabati wa vivuko pamoja na miundombinu yake ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Tawala cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020/2025.
Read More