Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Samia Akutana na Kuzungumza na Viongozi wa TLS Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma
Aug 14, 2023
Rais Samia Akutana na Kuzungumza na Viongozi wa TLS Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati alipokutana na Viongozi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 14 Agosti, 2023.
Na Ikulu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Harold Sungusia Hati ya Kiwanja kilichopo Arusha kwa ajili ya Ujenzi wa Ofisi zao mara baada ya mazungumzo yao Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 14 Agosti, 2023.

 

Viongozi pamoja baadhi ya Wanachama wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) pamoja na Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS) wakiwa kwenye Kikao na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 14 Agosti, 2023.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, Mwanasheria Mkuu wa Serikalii, Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi, Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Harold Sungusia pamoja ns ujumbe wake katika picha ya pamoja mara baada ya mazungumzo yao Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 14 Agosti, 2023.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi