Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, Ndg. Juma Ali Khatib akisoma maazimio yatokanayo na mkutano wa Baraza hilo uliofanyika tarehe 1 Agosti, 2023 jijini Dar es Salaam mbele ya Waandishi wa Habari mara baada ya kumaliza Kikao cha Kamati ya Uongozi wa Baraza hilo leo tarehe 16 Agosti, 2023 jijini Dodoma. Kikao hicho kilichokuwa na ajenda ya kupitia maazimio hayo na maandalizi ya Mkutano Maalum wa Baraza hilo unaotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 28 hadi 30 Agosti, 2023. Kulia ni Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Mohamed Ali Ahmed na Msajili Msaidizi Sisty Nyahoza.
Read More