Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewaagiza Mabalozi aliowaapisha wakawajibike ipasavyo ili kuleta tija katika nchi.
Agizo hilo amelitoa leo katika hafla ya uapisho wa Mabalozi hao wateule iliyofanyika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.
“Uteuzi wenu huu ni dalili tosha ya imani kubwa ya taifa iliyonayo kwenu ya kuiwakilisha Tanzania katika nchi nyingine pamoja na taasisi na Jumuiya za kimataifa” amesema Rais Samia.
Mhe. Rais Samia aliendelea kwa kusisitiza “Nataka mfahamu kwamba dhamana na majukumu mliyopewa ni kubwa na mazito mkaiwakilishe vizuri Tanzania katika nafasi hiyo”.
Aidha, Mhe. Rais Samia amesema Tanzania haiwezi kufanya kazi pekee yake, inahitaji kushirikiana na mataifa mengine kwa kuwa nayo yanaihitaji ili kukuza ushirikiano na utengamano katika mambo mbalimbali.
Kuhusu mahitaji mapya duniani Rais Samia ameyataja baadhi kuwa ni Mabadiliko ya Tabia nchi, Mapinduzi ya Nne ya Viwanda, Matumizi ya Akili Bandia, Uchumi wa Buluu, Umuhimu wa Madini ya Kimkakati, Utalii Endelevu,
Naye, Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa amewataka Mabalozi wateule kutambua Diplomasia ya nchi ya kisiasa, kiuchumi pia kibiashara inahitaji kuimarika zaidi hasa wakijua kuwa sera ya nchi ni kuimarisha uchumi wa ndani.