Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili na Uhusiano ya Baraza la Vyama vya Siasa, Ndg. Doyo Hassan Doyo akichangia mada wakati wa kikao cha Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa kilichofanyika leo tarehe 16 Agosti ,2023 jijini Dodoma. Kikao hicho kilikuwa na ajenda ya kupitia maazimio hayo na maandalizi ya Mkutano Maalum wa Baraza hilo unaotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 28 hadi 30 Agosti, 2023. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Masuala ya Bunge na Siasa, Ndg. Abdul Mluya na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili na Uhusiano, Ndg. Mohamed Omari Shaame.Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Utawala Bora ya Baraza la Vyama vya Siasa, Ndg. Rashid Mohamed Rai akichangia mada wakati wa kikao cha Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa kilichofanyika leo tarehe 16 Agosti 2023 jijini Dodoma.
Giza
Mwanga
Chaguo Msingi
Ndogo
Kawaida
Kubwa