WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka maaafisa na makamanda wa Jeshi la Magereza nchini waendelee kusimamia haki na usawa wanapotimiza wajibu wao.
Ametoa wito huo leo jioni (Jumatatu, Juni 12, 2017) wakati akizungumza na maafisa na makamanda wa jeshi hilo katika hafla ya kuwavisha vyeo maafisa 29 iliyofanyika kwenye viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCTA), Ukonga, jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu ambaye amefanya kazi hiyo kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, amewavisha vyeo maafisa watano kuwa Naibu Kam...
Read More