Na Jonas Kamaleki.
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imepima viwanja 4333 hadi mwishoni mwa Mei, 2017 ambapo hatua za umilikishaji zimeanza kutekelezwa ili kurasimisha maeneo yaliyojengwa kiholela jijini Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Mipango Miji na Vijiji wa Wizara hiyo, Bertha Mlonda katika maohojiano maalum na mwandishi wahabari hii.
Kwa mujibu wa Mlonda, jumla ya viwanja 6,000 vinatarajiwa kupimwa na kumilikishwa katika jiji la Dare es Salaam katika zoezi zima la urasimishaji wa makazi...
Read More