Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amempongeza mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Watoto (UNICEF) kwa kazi kubwa iliyofanywa na Shirika hilo hapa nchini.
Ametoa pongezi hizo leo (Alhamisi, Aprili 11, 2019) alipokutana na mwakilishi wa UNICEF, Bibi Maniza Zaman ofisini kwake Magogoni, jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu amempongeza Bibi Zaman kwa upendo mkubwa aliouonesha kwa watoto wa Tanzania hasa katika kusimamia masuala ya afya, elimu na haki za watoto wa kike. “Tumenufaika na mengi kutoka UNICEF wakati ukiwa hapa hasa kwenye masuala ya h...
Read More