Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Desemba 28, 2023 ametunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Heshima ya Usimamizi wa Utalii na Masoko (Doctor of Philosophy in Tourism Management and Marketing (Honoris Causa)) na Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) visiwani Zanzibar. Ametunukiwa shahada hiyo na Mkuu wa chuo hicho, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Read More