Na: Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma
Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameahidi kulipa madeni ya walimu takribani shilingi Bil. 25 mara baada ya viongozi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kuthibitisha uhalali wa madeni hayo.
Rais Dkt. Magufuli ametoa tamko hilo leo Mjini Dodoma ,alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa CWT ambao umehusisha wawakilishi kutoka Mikoa yote ya Tanzania Bara .
"Ninawaahidi walimu wenzangu, mara baada ya zoezi la uhakiki kuisha wale walimu ambao wanadai malipo halali watalipwa," alifafanua Rais Dkt. Magufuli.
Aliendelea...
Read More