Na: Lilian Lundo
Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri, Manispaa na Majiji, Mameya na Wenyeviti wa Halmashauri wamempongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa maamuzi anayoyafanya katika kutetea rasilimali za nchi pamoja na kuwatetea wanyonge.
Pongezi hizo zimetolewa leo Mjini Dodoma na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri kwa niaba ya viongozi hao alipokuwa akifunga Warsha ya Kitaifa Juu ya Maboresho ya Huduma za Umma na Ugatuaji wa Madaraka kwenye Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa uliohusisha Wakuu wa Mik...
Read More