Watumishi wa Umma wapatao 440 wanatarajiwa kuondoka nchini kwenda Korea Kusini kupata mafunzo ya muda mfupi ili kuongeza ujuzi katika kazi zao.Watumishi hao ni wale wanaofanya kazi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika sekta mbalimbali ikiwamo afya, nishati, maji na nyinginezo katika ulimwengu wa leo ambapo mifumo ya kidijitali inatumika katika kutoa huduma zote kwa jamii.Akizungumza leo jijini Dodoma, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Ndg. Mohamed Hamisi Abdulla amesema idadi hiyo ni sehemu...
Read More