Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison G. Mwakyembe (Mb) amepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mwanamuziki nguli wa Muziki wa Dansi nchini Bw. Abdallah Mgonahazeru aliyefariki dunia jana jijini Dar es Salaam.
Hadi anafikwa na umauti, Bw. Mgonahazeru alikuwa Kiongozi wa Bendi ya Vijana Jazz (SAGA RHUMBA). Marehemu pia amewahi kuwa Mwanamuziki katika Bendi za Cuban Marimba pamoja na Madevela Sound.
Waziri Mwakyembe ametoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki, Uongozi wa Vijana Jazz, Uongozi Cham...
Read More