Rais Samia Ahutubia Jukwaa la Wafanyabiashara, Ashuhudia Utiaji Saini Hati za Makubaliano
Jul 18, 2021
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Rais wa Jamhuri ya Burundi, Mhe. Evariste Ndayishimiye pamoja na Mkewe baada ya kuhudhuria Dhifa ya Jioni iliyoandaliwa na Rais Evariste Ndayishimiye wa Burundi Ikulu Bujumbura Burundi leo Julai 16,2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Burundi, Mhe. Evariste Ndayishimiye wakipokea heshima ya wimbo wa Taifa walipowasili katika Ukumbi wa Royal Jijini Bujumbura kwa ajili ya kuhutubia katika Jukwaa la Wafanyabiashara wa Tanzania na Burundi lililofanyika leo Julai 17,2021. ambapo Mhe. Rais Samia amekamilisha ziara yake ya siku mbili Nchini Burundi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia kwenye mkutano wa Jukwaa la Wafanyabiashara wa Tanzania na Burundi uliofanyika leo Julai 17,2021 Jijini Bujumbura Nchini Burundi. ambapo Mhe. Rais Samia amekamilisha ziara yake ya siku mbili Nchini Burundi.
-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Jamhuri ya Burundi, Mhe. Evariste Ndayishimiye, wakishuhudia utiaji saini hati 8 za makubaliano kati ya Nchi mbili hizi leo Julai 16,2021.