Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Kyaka Misenyi mkoani Kagera (hawapo pichani) wakati akielekea Wilayani Karagwe.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bukoba mara baada ya kuzungumza nao.
Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko na Msajili wa Hazina Bw. Athumani Mbuttuka (wa tatu toka kushoto walioketi) pamoja na wanasheria wakishuhudia Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt Adelardus Kilangi na Makamu wa Rais wa Kampuni ya LZ NICKEL LIMITED ya Uingereza Bw. Chris Von Chritierson wakitia saini makubaliano ya pamoja ya ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kampuni hiyo katika uchimbaji wa madini ya Nickel katika mgodi wa Kabanga wilayani Ngara mkoa wa Kagera
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Msajili wa Hazina, Bw. Athumani Mbuttuka akibadilishana nyaraka na Makamu wa Rais wa Kampuni ya LZ NICKEL LIMITED Bw. Chris Von Christierson baada ya kutiliana saini makubaliano ya ushirikiano katika uchimbaji wa madini ya Nickel huko Kabanga katika Wilaya ya Ngara mkoani Kagera kwenye hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Bukoba mjini Bukoba leo Jumanne Januari 19, 2021
Msajili wa Hazina, Bw. Athumani Mbuttuka akionesha nyaraka akiwa na
Makamu wa Rais wa Kampuni ya LZ NICKEL LIMITED, Bw. Chris Von Christierson (katikati) na afisa wa kampuni ya LZ NICKEL LIMITED baada ya kutiliana saini makubaliano ya ushirikiano katika uchimbaji wa madini ya Nickel huko Kabanga katika Wilaya ya Ngara mkoani Kagera kwenye hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Bukoba mjini Bukoba leo Jumanne Januari 19, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki akiweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kusindika maziwa na vyakula vya mifugo cha Kahama Fresh mjini Karagwe unaoendeshwa na mwekezaji mzawa Bw. Jossam Ntangeki leo Jumanne Januari 19, 2021
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi wengine akisikiliza maeleo ya mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kusindika maziwa na vyakula vya mifugo cha Kahama Fresh mjini Karagwe kabla ya kuweka jiwe la msingi la mradi huo utaondeshwa na mwekezaji mzawa Bw. Jossam Ntangeki leo Jumanne Januari 19, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli akiwa Mkurugenzi wa kampuni ya Kahama Fresh, Bw. Jossam Ntageki baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kusindika maziwa na vyakula vya mifugo cha Kahama Fresh mjini Karagwe baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi huo utaondeshwa na mwekezaji huyo mzawa leo Jumanne Januari 19, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kusindika maziwa na vyakula vya mifugo cha Kahama Fresh mjini Karagwe unaoendeshwa na mwekezaji mzawa Bw. Jossam Ntangeki leo Jumanne Januari 19, 2021.