Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Ziara ya Dkt. Shein Dubai
Jan 24, 2018
Na Msemaji Mkuu

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein na Mkewe   Mama Mwanamwema Shein, wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Bandari ya Jebel Ali Port and Free Zone Dubai akitowa maelezo ya picha za muonekano wa Bandari hiyo inayotoa huduma za kupakia mizigo na kushusha wkati alipofanya ziara katika bandari hiyo Nchini Dubai. (Picha na Ikulu Zanzibar)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Mfalme na Mtawala wa Dubai, Shaikh Mohammed Bin Rashid Al Maktoum alipofika katika makaazi ya Mfalme huyo Nchini Dubai akiendelea na ziara yake ya kiserikali katika Nchi za Umoja wa Falme za Nchi za Kiarabu. (Picha na Ikulu Zanzibar)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa Mradi wa Nakheel, Sanjey Machanda akitowa maelezo ya picha mbalimbali wakati wa kutembelea mradi huo. (Picha na Ikulu Zanzibar)

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi