Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wizara Yapokea Kompyuta Sita Kutoka SOS, Kuboresha Utendaji Kazi
Oct 07, 2022
Na Jacquiline Mrisho


Na MJJWM, Dodoma


Shirika la Children's SOS Village limeikabidhi Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Kompyuta sita zenya thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 14 aina ya HP Brobook  shabaha ikiwa ni kuboresha utendaji kazi wa kila siku kwa wataalam wa Wizara hiyo.

Hafla ya Mapokezi hayo imefanyika leo Oktoba, 07, 2022 na kuongozwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara, Patrick Golwike, katika Ofisi za Wizara zilizopo Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambapo Menejimenti na wataalam kutoka Wizara hiyo, wameshuhudia mapokezi hayo huku wakilipongeza Shirika hilo kwa mchango wake wanaoendelea kuutoa kwa Serikali.


Akipokea Kompyuta hizo, Kaimu Katibu Mkuu Golwike amewashukuru SOS kwa msaada huo na misaada mingine ambayo Shirika hilo imekuwa ikiitoa katika maeneo mbalimbali nchini kwa ajili ya kuboresha huduma kwa jamii ya watanzania.

“Mlichokileta hapa leo sio kidogo, ni kikubwa sana kwani upatikanaji wa kompyuta hizo utachochea na kumfanya mfanyakazi kufanya kazi zake muda wote na mahali popote akiwa na Kompyuta kwani kweli bado tunauhitaji kutokana na mabadiliko  ya Teknoljia", amesema Golwike.


Aidha, Golwilke amewataka watumishi watakaopata sehemu ya Kompyuta hizo kuzitunza na kufanyia kazi kwa malengo yaliyokusudiwa ikiwepo kuboresha kazi zao.


Naye Mkurugenzi wa Shirika hilo, David Mulongo, amesema Dunia ikiwa inahama na kuachana na matumizi ya makaratasi wameona ni muda muafaka wa kurahisisha utendaji kwa kuunga mkono jitihada mbalimbali zinazofanywa kwa kutoa vitendea kazi kwa Wizara ili watumishi wake waweze kutekeleza majukumu yao.


“Dunia ikiwa inahama kutoka kwenye 'paper work' na kuhamia kwenye 'paperless' ni wakati muafaka pia kuboresha utedaji wa kazi, tulipokea maombi ya kufanya uwezeshaji wa vitendea kazi nasi kwa SOS tukaona ni wakati muafaka“, amesema Mulongo.


Awali akimkaribisha Kaimu Katibu Mkuu kuzungumza, Kamishna wa Ustawi Msaidizi wa Jamii, Baraka Makona alisema SOS Children’s wameendelea kuwa wa mfano katika kushirikiana na Serikali na kutoa michango yao ya hali na mali ili kuwawezesha wataalam wa Serikali.


Katika hatua nyingine, Bwana David Mulongo amewaambia wajumbe waliohudhuria hafla hiyo kuwa kwa sasa wamekamilisha andiko litakalo kwenda kutatua changamoto za watoto waishio na kufanya kazi mtaani.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi