Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Maliasili na Utalii Yakabidhiwa Rasimu ya Mwisho ya Sera ya Taifa ya Misitu
Apr 10, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_30158" align="aligncenter" width="800"] Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen Gaudence Milanzi (wa kwanza kulia) akikabidhiwa nakala ya Rasimu ya mwisho ya Sera ya Taifa ya Misitu na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) hapa nchini, Fred Kafeero (wa pili kushoto) katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika makao makuu ya ya Wizara mjini Dodoma. Wa kwnza kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki.[/caption]

Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imekabidhiwa rasimu ya mwisho ya sera ya Taifa ya Misitu na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO)  kufuatia kukamilika kwa mchakato uliowashirikisha wadau wote muhimu.

Hatua hiyo inafuatia ikiwa ni mwaka mmoja sasa ambapo FAO na wizara ya Maliasili na Utalii ziliposainiana mkataba wa msaada wa Kitaalamu kuisaidia serikali kukamilisha mapitio ya Sera ya Taifa  ya Misitu ambayo ilipitishwa mwaka 1998.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen Gaudence Milanzi  amesema  Tanzania inakabiliwa na changamoto katika kuthibiti rasilimali misitu kwa kuwa sera ya misitu inayotumika kwa sasa ni ya zamani hali inayochangia kushindwa kuendana na kasi ya  maendeleo  sasa.

[caption id="attachment_30161" align="aligncenter" width="800"] Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa akizungumza mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen Gaudence Milanzi na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) hapa nchini, Fred Kafeero (wa pili kushoto) kabla ya makabidhiano ya Rasimu ya mwisho ya Sera ya Taifa ya Misitu katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika makao makuu ya ya Wizara mjini Dodoma.[/caption]

Ameyasema hayo leo tarehe  10 April, 2018 katika hafla ya makabidhiano hayo iliyofanyika katika makao makuu ya Wizara mjini Dodoma baina yake, na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) hapa nchini, Fred Kafeero.

Milanzi amesema msaada huo umekuja kwa wakati muafaka wakati ambapo nchi inakabiliwa na changamoto nyingi za uharaibifu wa misitu.

‘’Tunahitaji sera dhabiti ya kukabiliana na masuala mbalimbali yanayohusu uharibifu wa rasilimali za misitu’’ alisisitiza Milanzi.

Kwa upande wake, Kafeero alisema alisema FAO imepiga hatua kubwa za mafanikio katika kukamilisha  mchakato wa kuandaa rasmu hiyo ambayo ni shirikishi.

[caption id="attachment_30159" align="aligncenter" width="800"] Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen Gaudence Milanzi ( wa kwanza kulia) akizungumza mara baada ya makabidhiano ya nakala ya Rasimu ya mwisho ya Sera ya Taifa ya Misitu katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika makao makuu ya ya Wizara mjini Dodoma. Wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki.[/caption] [caption id="attachment_30160" align="aligncenter" width="800"] Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) hapa nchini, Fred Kafeero (wa pili kushoto) akizungumza mara baada ya makabidhiano ya nakala ya Rasimu ya mwisho ya Sera ya Taifa ya Misitu katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika makao makuu ya ya Wizara mjini Dodoma. Wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki.[/caption]

‘’Tayari FAO imesaidia nchi nyingi kwenye maeneo hayo lengo likiwa kuhakikisha kuwa sera hiyo inatilia maanani masuala ya maendeleleo ya kitaifa na kimataifa.

Aidha, Kafeero alisema misitu ni moja ya maeneo ya majukumu makuu ya FAO kwa kuwa ni moja ya maeneo muhimu yanayohusiana na matumizi endelevu ya maliasili, uhakika wa chakula na lishe pamoja na maendeleo ya uchumi kwa ujumla.

Wakati huo huo, FAO pamoja na Serikali wanamalizia taratibu za kuandaa mkakati wa kuitekeleza  Sera hiyo ili  iweze kuleta matokeo chanya yaliyokusudiwa katika misitu nchini.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi