Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wizara ya Habari Yashauriwa Kuelimisha Jamii Juu ya Matumizi Sahihi ya Muda
Jul 11, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_6175" align="aligncenter" width="800"] Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka (kulia) alipofanya ziara ya kutembelea Mkoa huo.[/caption]

(Picha na Zawadi Msalla-WHUSM)

Na Zawadi Msalla-WHUSM

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka  amewataka  watendaji wa Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo kuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu  kwa umma ya kuwa na utamaduni wa kutumia muda kimkakati ili kufanya kazi kwa bidii  na kufikia malengo.

Ayasema hayo wakati wa mkutano na watendaji hao  walipomtembelea ofisini kwake wakati wa ziara ya kutembelea mikoa ya Kusini mwa Tanzania kwa lengo la kutembelea maeneo mbalimbali yanayojihusisha uhifadhi wa utamaduni usioshikika kama vile Mila na Desturi za Watanzania.

“Utamaduni wa kutumia muda kimkakati ni muhimu kwa Taifa na mtu binafsi kwa kuwa inasaidia katika kuweka motisha ya kufanya kazi kwa bidii na hivyo kufikia lengo lililokusudiwa” alisema Mhe. Ole Sendeka.

Aidha aliongeza  kuwa falsafa ya mabadiliko ya utamaduni chanya ya ufanyaji kazi ilianza tangu awamu ya kwanza ya uongozi wa  hayati Mwl. Nyerere iliyokwenda kwa jina la Uhuru na Kazi na baadaye ikifuatiwa na kazi ni kipimo cha Utu ambapo katika utawala wa awamu hii ya tano inaongozwa na falsafa ya Hapa Kazi tu lengo ikiwa ni kufanya kazi kwa ajili ya kukuza uchumi wetu.

Mhe. Ole Sendeka anaeleza kuwa dhumuni za falsafa hizo ni kuhakikisha kuwa kila mtu anatimiza wajibu wake wa kutumia muda kimkakati kwa kufanya kazi ili kujenga Taifa bora lenye maendeleo.

“Endapo elimu ya kutosha ya utamaduni wa kufanya kazi itatolewa ni imani kuwa azma ya Mhe. Rais ya kuwatoa watanzania katika uchumi ulio nyuma na tegemezi kwa kuwapeleka katika uchumi wa kisasa wa taifa linalojitegemea itawezekana” alisema Mhe. Ole Sendeka.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante  Ole Gabriel aliahidi kufanyia kazi mawazo hayo kwa kuhakikisha jamii inapata elimu ya kutosha namna ya kuwa na utamaduni wa kutumia muda kimkakati kwa kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Pia alieleza kwamba  ni kweli usiopingika ili  Taifa  liweze kufikia uchumi wa viwanda ni budi kwa wananchi wake kujengea utamaduni wa kufanya kazi kwa bidi ikiwemo kutumia muda kimkakati.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi