[caption id="attachment_51929" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa studio mpya ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) inayojengwa katika eneo la ofisi hizo zilizopo Mikocheni. Programu Tumizi (App) ya Safari Channel pamoja na mfumo mpya wa upashanaji habari unaofahamika kama TBC Aridhio. Hafla hiyo ilifanyika tarehe 30 Machi, 2020 Mikocheni jijini Dar es salaam.[/caption]
Na Mwandishi Wetu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka watangazaji na watumishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kuongeza weledi na kujituma ili wengine wapate kuiga mambo mazuri kutoka kwao.
Waziri Mwakyembe ameyasema hayo jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa studio mpya ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) inayojengwa katika eneo la ofisi hizo zilizopo Mikocheni.
Aidha, Dkt. Mwakyembe alizindua Programu Tumizi (App) ya Safari Channel pamoja na mfumo mpya wa upashanaji habari unaofahamika kama TBC ARIDHIO ambapo neno Aridhio linamaanisha taarifa au habari.
[caption id="attachment_51927" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Habari, Utamadumi, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akikata utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa studio ya televisheni ya Taifa (TBC) kwa ajili ya uboreshaji wa mundombinu ya utangazaji. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Hassan Abbasi na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dkt. Ayub Rioba.[/caption]“Tuna deni kubwa la kuhakikisha tunaongeza weledi na kujituma, hivyo kuendelea kuwa kiongozi wa habari hapa nchini, lazima TBC kiwe ni chombo cha rejea, wakitangaza wengine mtu awe na shauku ya kujua TBC imesema nini kwanza”, amesema Dkt. Mwakyembe.
[caption id="attachment_51926" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi akiongea wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa studio mpya ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) inayojengwa katika eneo la ofisi hizo zilizopo Mikocheni. Programu Tumizi (App) ya Safari Channel, pamoja na mfumo mpya wa upashanaji habari unaofahamika kama TBC Aridhio. Hafla hiyo ilifanyika tarehe 30 Machi,2020.[/caption] [caption id="attachment_51928" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) akizungumza wakati wa hafla hiyo ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa studio mpya ya shirika hilo inayojengwa katika eneo la ofisi hizo zilizopo Mikocheni. Programu Tumizi (App) ya Safari Channel, pamoja na mfumo mpya wa upashanaji habari unaofahamika kama TBC Aridhio. Hafla hiyo ilifanyika tarehe 30 Machi,2020.[/caption]Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Hassan Abbasi amewapongeza wafanyakazi wa Shirika hilo kwa hatua hiyo kubwa ya kuleta mapinduzi na ubunifu katika tasnia ya habari katika chaneli hiyo ya Tanzania inayotegemewa na taifa.
Mabadiliko haya makubwa ya upashanaji habari ndani ya TBC yanakuja baada ya miaka 13, ambapo safari hii ilianza mwaka 2007.
Ujenzi wa jengo hilo la kisasa umeanza Februari, 2020 na utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 2.38/- na unatarajiwa kukamilika Agosti 2020, ambapo hadi sasa ujenzi huo umefikia asilimia 20.
[caption id="attachment_51925" align="aligncenter" width="750"] Mwalimu wa Kiswahili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Elizabeth Mahenge akizungumza wakati wa uzinduzi huo. Elizabeth Mahenge ndiye aliyekuja na neno ARIDHIO ambapo amesema neno ARIDHIO ni kisawe cha neno taarifa na pia ni kisawe cha neno Habari.[/caption]Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mfumo huo mpya wa upashanaji habari Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dkt. Ayoub Rioba amesema kuwa kutokana na mahitaji ya sasa ya dunia ya sayansi na teknolojia imelazimika mifumo ya zamani ya upashanaji habari kupinduliwa na kuja na namna mpya za upashanaji habari.
Aidha Dkt. Ayoub Rioba ameishukuru Wizara kwa namna ambavyo imekuwa bega kwa bega katika kuunga mkono mafanikio ya Shirika hilo.