Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri wa Katiba na Sheria, Atembelea Mahakama
Jul 14, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_6532" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi (pichani) akiongea na Watendaji wa Mahakama pindi alipotembelea Mahakama ya Rufani (T) mapema leo na kuonana na Kaimu Jaji Mkuu na Viongozi wengine wa Mahakama,Prof. Kabudi amehaidi kutoa ushirikiano wa dhati kwa Mahakama katika utekelezaji wake wa jukumu la utoaji haki nchini, katikati ni Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma, kulia ni Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali.[/caption]

Na Lydia Churi-Mahakama

Mahakama ya Tanzania inayo nafasi kubwa katika kujenga uchumi wa viwanda kwa kuhakikisha inamaliza kwa wakati kesi hasa zile zinazohusu masuala ya kodi ili kuharakisha maendeleo ya nchi.

Akizungumza leo alipotembelea Mahakama ya Tanzania, Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi ameitaka Mahakama kuimarisha uadilifu na uwajibikaji ili wananchi wapate haki zao kwa wakati.

[caption id="attachment_6535" align="aligncenter" width="750"] 2. Viongozi na Watendaji mbalimbali wa Mahakama ya Tanzania na Wizara ya Katiba na Sheria wakimsikiliza Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi pindi alipokuwa akitoa hotuba yake pindi alipotembelea Mahakama ya Rufani mapema Julai, 14, 2017, Mhe. Kabudi amempongeza Mhe. Kaimu Jaji Mkuu kwa kuteuliwa kwake kushika nafasi hiyo, hii ni mara ya kwanza Waziri kutembelea Mahakama tangu kuteuliwa kwake kushika nafasi ya Uwaziri, Machi 24, 2017.[/caption]

Aidha, Prof. Kabudi alisema anatambua na kuipongeza Mahakama kwa kupanga  mikakati ya kuziondosha mahakamani kesi zote za muda mrefu pamoja na kusogeza huduma kwa wananchi kwa kujenga na kukarabati baaadhi ya majengo  Mahakama.

Akizungumzia suala la rushwa ndani ya Mahakama, Prof. Kabudi amewataka viongozi wa mahakama kushughulikia suala hilo bila uwoga wala upendeleo.

Wakati huo huo, Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma amesema Mahakama itaendelea kushirikiana kwa karibu na mihimili mingine ya nchi ili kuharakisha maendeleo ya nchi.

[caption id="attachment_6537" align="aligncenter" width="750"] 3. Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma (katikati) akiongea na Watendaji wa Mahakama na Wizara (hawapo pichani) pindi Waziri alipotembelea Mahakama, wa kwanza kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, wa kwanza kulia ni Jaji Kiongozi-Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali.[/caption] [caption id="attachment_6538" align="aligncenter" width="750"] Kaimu Jaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma (kulia) akimkabidhi vitabu vya Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania pindi alipotembelea Mahakama ya Rufani mapema leo.[/caption]

Akizungumzia kuhusu sheria, Prof. Juma alisema falsafa ya ni kwa namna gani sheria zinufaishe uchumi wa watanzania ni muhimu kwa kuwa sheria zina mchango katika wa uchumi wa nchi na zinasaidia katika kuondoa umaskini.

Kaimu Jaji Mkuu pia alimshauri Waziri wa katiba na Sheria kutumia Sheria kuinua watanzania wengi hasa wale wenye hali duni za maisha kwa kuwa sheria hutumika katika ukuaji wa uchumi na maendeleo ya nchi.

[caption id="attachment_6544" align="aligncenter" width="750"] Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga akiendelea kutoa mada kupitia 'Projector.'[/caption] [caption id="attachment_6545" align="aligncenter" width="800"] Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali (aliyesimama) akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Katiba na Sheria, mara baada ya majadiliano kukamilika.[/caption] [caption id="attachment_6546" align="aligncenter" width="800"] Kaimu Jaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi na Watendaji wa Mahakama na Wizara mara baada ya kukamilika kwa majadiliano na Waziri wa Katiba na Sheria alipotembelea Mahakama mapema leo, wa tatu kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, wa kwanza kulia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani (T), Mhe. Sauda Mjasiri, wa kwanza kushoto ni Jaji wa Mahakama ya Rufani (T), Mhe. Mussa Kipenka, wa tatu kulia ni Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali, wa pili kushoto ni Katibu Mkuu, Wizara ya Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Sifuni Mchome na wa pili kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara wa Katiba na Sheria, Mhe. Amon Mpanju. (Picha na Mary Gwera, Mahakama)[/caption]

Naye Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali alisema Mahakama ya Tanzania imefanikiwa katika utendaji kazi wake kwa kuwa hivi sasa asilimia 72 ya mashauri yaliyofunguliwa kwenye mahakama mbalimbali nchini pamoja na yale muda mrefu yamemalizika.

Alisema Mahakama imekuwa ikiyamaliza kwa haraka mashauri yote yanayohusu miradi mikubwa licha ya idadi ndogo ya Majaji waliopo.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi