Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Ummy Azindua Benki Ya Damu MOI
Nov 03, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_21639" align="aligncenter" width="750"] Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu aliyesimama akiongea na baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Mifupa nchini MOI wakati wa uzinduzi wa Benki ya damu iliyodhaminiwa na Ubalozi wa Kuwait leo jijini Dar es salaam, Kulia ni Balozi wa Kuwait Bw. Jasem Ibrahim Al-Najem.

[/caption] [caption id="attachment_21640" align="aligncenter" width="750"] Balozi wa Kuwait Bw. Jasem Ibrahim Al-Najem aliyesimama akiongea na baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Mifupa nchini MOI wakati wa uzinduzi wa Benki ya damu iliyodhaminiwa na Ubalozi wa Kuwait leo jijini Dar es salaam , katikati waliokaa ni Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na anayefuata ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Dkt. Respicious Lwezimula.[/caption]

Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (MB) amezindua benki ya kisasa ya damu katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI. Benki hiyo yenye vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 220 imefadhiliwa na ubalozi wa Serikali ya Kuwait nchini Tanzania.

Akizungumza wakati wa uzinduzi Mh Mwalimu amesisitiza damu kutolewa bure kwa wagonjwa. “Watanzania wanahoitaji huduma ya kuongezewa damu wapewe bure, ni marufuku kwa watoa huduma za vituo vya afya pamoja na hospitali zote kuuza damu hiyo kwani inatoka kwa wananchi wenyewe”

  [caption id="attachment_21641" align="aligncenter" width="750"] Balozi wa Kuwait Bw. Jasem Ibrahim Al-Najem kulia akimkabidhi zawadi ya mchango mkubwa katika Wizara ya Afya Mhe. Ummy Mwalimu kushoto wakati wa uzinduzi wa Benki ya damu iliyodhaminiwa na Ubalozi wa Kuwait leo jijini Dar es salaam.
[/caption] [caption id="attachment_21642" align="aligncenter" width="750"] Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizindua Benki ya damu iliyodhaminiwa na Ubalozi wa Kuwait leo jijini Dar es salaam akiwa na Balozi wa Kuwait Bw. Jasem Ibrahim Al-Najem.
[/caption] [caption id="attachment_21643" align="aligncenter" width="750"] Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizindua Benki ya damu iliyodhaminiwa na Ubalozi wa Kuwait leo jijini Dar es salaam akiwa na Balozi wa Kuwait Bw. Jasem Ibrahim Al-Najem.[/caption]

Pia, Waziri Mwalimu amesewaasa wananchi kujitokeza katika kuchangia damu ili   hifadhi ya damu iwe ya kutosha na hivyo wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo kuipata kwa wakati sahihi bila ya usumbufu wowote katika kuokoa maisha ya watanzania.

Kwa upande wake Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Bw. Jasem Ibrahim Al-Najem amesema kuwa wameamua kuchangia kiasi cha fedha cha shilingi Milioni 220 katika kutengeneza Benki hiyo ya damu MOI ili kuweza kusaidia kuboresha sekta ya afya nchini.

“Mbali na kiasi hicho cha fedha pia tumetoa Dola za Kimarekani 500 ili kuweza kusaidia  walemavu mbalimbali katika kulejesha hali zao za kawaida hapa nchini” alisema Bw. Al-Najem.

[caption id="attachment_21644" align="aligncenter" width="750"] Balozi wa Kuwait Bw. Jasem Ibrahim Al-Najem akichangia damu katika Benki ya damu mpya iliyozinduliwa na Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi huo uliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
[/caption] [caption id="attachment_21645" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa MOI Dkt. Respicious Lwezimula aliyesimama akiongea na baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Mifupa nchini MOI wakati wa uzinduzi wa Benki ya damu iliyodhaminiwa na Ubalozi wa Kuwait leo jijini Dar es salaam, kulia aliyekaa ni Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.[/caption]

Aidha, Balozi Al-Najem alijitolea damu chupa moja ili  kuhamasisiha wananchi wengine waweze kuchangia damu na pia kutoa msaada kwa wagonjwa wengine wanaohitaji msaada.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Respicious Lwezimula alisema kuwa katika kuhakikisha Matibabu ya kibingwa yanapiga hatua hapa nchini na hivyo MOI ilianzisha kambi za matibabu kuanzia mwaka 2000 na kufanya taasisi zingine za afya hapa nchini kuiga mfano huo.

“Tunataka kuhamasisha matibabu ya kibingwa kufanyika nchini pamoja na uchangiaji damu kwani damu hiyo haitatumika MOI peke yake bali hata kwenye Taasisi zingne na vituo vya Afya nchini kote” alisema Dkt. Lwezimula.

Sambamba na tukio hilo Kikundi cha Kutayarisha Madereva wa Magari Makubwa  Wanawake (Women on Wheel) Afrika Mashariki walijitolea kuchangia damu ili kuunga mkono jitihada za Serikali na pia kuwasaidia wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo ya damu.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi