Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Simbachawene, Ahimiza Mafunzo ya Itifaki Kuwa Endelevu
Nov 20, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na Mwandishi wetu

Waziri wa Nchi wa Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. George Simbachawene amesema ipo haja mafunzo ya itifaki na uratibu wa maadhimisho kufanyika kila mwaka.

Wito huo umetolewa Mhe. George Simbachawene wakati akifunga mafunzo kwa Watendaji wa Serikali yaliyohusu itifaki ya viongozi wa kitaifa iliyowakutanisha Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu na Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa yaliyofanyika mkoani Singida tarehe 19/11/2022.

“Mafunzo haya yanapaswa kuongezwa mada na kuongeza namba ya washiriki ili kujenga uelewa wa pamoja.”

Ambao utasaidia kupata ufahamu na ujuzi muhimu wa namna ya uandaaji wa Maadhimisho yanayohusu Idara na Taasisi za Serikali kwa Viongozi Wakuu wa Kitaifa na kuzijua kanuni za kiitifaki ambazo mtazitumia katika uendeshaji wa shughuli mbalimbali kwenye taasisi zenu.

Awali, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge na Uratibu, Kaspar Mmuya amesema mafunzo yamelenga kuwa na utaratibu ambao umekubaliwa, ambao unaleta matokeo chanya na watu wote kuheshimu.

“Watendaji waliopokea mafunzo sasa watasaidia katika maeneo yao hasa kitengo cha maadhimisho Ofisi ya Waziri Mkuu, kwa sababu ndio Ofisi inayosimamia itifaki za viongozi”.

Naye Mtendaji Mkuu wa Mahakama Tanzania, Profesa Elisante Ole Gabriel aliyekuwa mtoa maada wa huduma bora kwa mteja ameishukuru Serikali kwa kuandaa mafunzo hayo ambayo yamesaidia kuwajenga watendaji kwenda kwa muelekeo unaolengwa na nchi.

“Huu ni uwekezaji wa kifikira unaofaa, watendaji wakitoa huduma bora kwa wananchi na kwa viongozi, mashauri yatapungua kwa sababu ya huduma kuwa nzuri.”

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi