Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Prof. Mbarawa Afungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi Shirika la Posta
Jan 29, 2018
Na Msemaji Mkuu

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Dk. Haruni Kondo (wa pili kulia), akibadilishana mawazo na Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa TPC, Joseph Ngowi (kulia), wakati wakimsubiri mgeni rasmi, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa. Katikati ni Kaimu Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe.Wengine kushoto ni Maofisa waandamizi kutoka wizarani.
Kaimu Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Posta, ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es Salaam leo. Wa pili kulia ni mgeni rasmi, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa.
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakisikiliza maelezo mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa katika ufunguzi huo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Mbarawa, akizungumza na wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Posta. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Posta, Dk. Haruni Kondo na kulia ni Kaimu Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe.
[caption id="" align="aligncenter" width="640"] Mjumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi, Ahmed Kaumo, ambaye pia ni Mwenyekiti TEWUTA, akitoa neno la shukrani kwa Waziri Prof. Mbarawa.[/caption]
[caption id="" align="aligncenter" width="640"] Mwenyekiti wa Bodi ya TPC Dkt. Haruni Kondo akisalimiana na wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi mara baada ya kuufungua mkutano wao huo jijini Dar es Salaam leo.[/caption]
[caption id="" align="aligncenter" width="640"] Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (katikati mbele), akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa TPC, mara baada ya kuufungua mkutano huo, jijini leo. kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya TPC, Dk. Haruni Kondo na kulia kwake ni Kaimu Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe.[/caption]
 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi