Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Ndalichako Ataka Muongozo wa SADC wa Kulinda Ajira kwa Watoto Kuzingatia Maadili ya Kiafrika
Mar 31, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na. Lusajo Mwakabuku, OWM-KVAU Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce  Ndalichako amewataka wajumbe wa mkutano wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuhakikisha katika mwongozo wa kulinda na kuzuia ajira mbaya kwa watoto ni vyema maneno yaliyotumika yakapatiwa tafsiri ili yaendane na maadili, utamaduni na mazingira ya kiafrika.

Waziri Ndalichako alitoa kauli hiyo leo jijini Lilongwe, Malawi alipokuwa akishiriki Mkutano wa Mawaziri wa Kazi na Ajira wa SADC waliokutana kujadili mambo mbalimbali juu ya sekta ya Kazi na Ajira ambapo katika kikao hicho ajenda 13 zinazohusu kuweka miongozo mbalimbali ya kusimamia masuala ya ukuzaji wa fursa za ajira, usimamizi wa viwango vya kazi, hifadhi ya jamii na usalama na afya mahala pa kazi.

Akitoa mchango wake, Prof. Ndalichako alisema suala la biashara ya ngono kwa mila na desturi ya nchi zetu za Afrika ni suala lisilokubalika, hivyo alisisitiza katika mwongozo huo isitafsiriwe kuwa biashara hiyo inakubalika kwa wasio watoto peke yake kwani kwa mazingira na tamaduni zetu za kiafrika biashara hiyo ni haramu.

Masuala mengine yaliyojadiliwa katika kikao hicho ni pamoja na kupitia rasimu ya Itifaki ya SADC ya Kazi na Ajira, Mwongozo wa kuanzisha Taasisi za Majadiliano ya Waajiri na Waajiriwa, Zana za Ufuatiliaji na Utoaji taarifa kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Uhamaji Nguvukazi ndani ya SADC pamoja na kuanzisha mfumo wa taarifa za soko la ajira wa SADC.

Pia mijadala mingine ilifanyika juu ya Hali ya Utekelezaji na Uridhiaji wa Itifaki na Mikataba ya Shirika la Kazi Duniani na pia mkutano huu ulipokea taarifa kuhusu maandalizi ya ushiriki wa nchi za SADC katika Mkutano Mkuu wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) unaotaratijwa kufanyika Mwezi Juni, 2022.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi