Waziri Ndalichako Akutana na Kufanya Mazungumzo na Ugeni Kutoka ILO
Feb 10, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani Ukanda wa Afrika Mashariki (ILO), Bw. Willington Chibebe (kushoto) alipomtembelea ofisini kwake Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma, februari 10, 2022.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (katikati) akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani Ukanda wa Afrika Mashariki (ILO), Bw. Willington Chibebe (kulia) alipomtembelea ofisini kwake Jijini Dodoma, Februari 10, 2022. Kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Prof. Jamal Katundu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani Ukanda wa Afrika Mashariki, Ndg. Willington Chibebe (kushoto) na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Prof. Jamal Katundu (kulia) katika eneo lililopandwa miti 100 wakati wa maadhimisho ya Miaka 100 ya shirika hilo yaliyofanyika 2019 Jijini Dodoma.