Waziri Nape Akutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Dodoma
Mar 24, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Selemani Kakoso (kulia) akimsikiliza Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye baada ya Waziri huyo kuwasilisha taarifa ya utekelezaji ya Wizara hiyo ya mwaka wa fedha 2021/2022 na bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023 kwa wajumbe wa Kamati hiyo kwenye ukumbi wa Bunge jijini Dodoma leo tarehe 24 Machi, 2022
Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mha. Kundo Mathew (wa katikati) akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Jim Yonazi (kushoto) wakati wa kikao cha kuwasilisha taarifa ya utekelezaji ya Wizara hiyo ya mwaka wa fedha 2021/2022 na bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023 kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kwenye ukumbi wa Bunge jijini Dodoma leo tarehe 24 Machi, 2022. Wa kwanza kulia ni Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Nape Nnauye (Mb)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi akifafanua jambo wakati wa kikao cha uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji ya Wizara hiyo ya mwaka wa fedha 2021/2022 na bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023 kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kwenye ukumbi wa Bunge jijini Dodoma leo tarehe 24 Machi, 2022.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (kulia) akifurahia jambo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Jim Yonazi baada ya Waziri huyo kuwasilisha taarifa ya utekelezaji ya Wizara hiyo ya mwaka wa fedha 2021/2022 na bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023 kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kwenye ukumbi wa Bunge jijini Dodoma leo tarehe 24 Machi, 2022.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi (kushoto) akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dkt. Ayoub Rioba baada ya kikao cha uwasilishaji taarifa ya utekelezaji ya Wizara hiyo ya mwaka wa fedha 2021/2022 na bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023 kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kwenye ukumbi wa Bunge jijini Dodoma leo tarehe 24 Machi, 2022.