Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknoolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye akiwa amekaa mbele ya studio za utangazaji za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) zilizopo jijini Dar es Salaam leo tarehe 09 Februari, 2022 katika ziara yake ya kikazi kwenye Shirika hilo.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye akisikiliza kwa makini maelezo ya utendaji kazi wa studio za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kutoka kwa Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi wa Shirika hilo, Mhandisi Upendo Mbelle katika ziara yake ya kikazi leo tarehe 09 Februari, 2022kwenye ofisi hizo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye akikagua vyombo vilivyopo kwenye studio ya kipindi cha Jambo Tanzania cha Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) wakati wa ziara yake ya kikazi kwenye ofisi za Shirika hilo lililopo jijini Dar es Salaam leo tarehe 9 Februari, 2022