Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Mwijage Mgeni Rasmi Tamasha la Magari.
Oct 25, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_21059" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Mtendaji wa Vision InvestmentS Bw. Ally Nchahaga (katikati) akieleza jambo juu ya Tamasha la Magari Tanzania (Autofest) mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Masoko kutoka Kampuni ya Bima ya Britam Insurance Bw. Oscar Ruhasha. Kulia ni Mkuu wa Mauzo na Masoko kutoka Kampuni ya Lake Oil Ltd, Bw. Aluwy Amar. Tamasha hilo litafanyika katika viwanja vya The Green Kenyatta Drive, Osterbay jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 27 hadi 29 mwaka huu.[/caption]

Na. Jacquiline Mrisho

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mh. Charles Mwijage ametarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tamasha la magari la Tanzania Automative Festival linaloandaliwa na Kampuni ya Vision Investiments.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Ally Nchahaga  alipokuwa akizungumza na  Waandishi wa Habari kuhusu lengo la kufanyika kwa tamasha hilo.

Nchahaga amesema kuwa tamasha hilo la siku mbili litakaloanza Oktoba 27 hadi 29 mwaka huu litafanyika katika viwanja vya The Green Kenyatta Drive vilivyopo eneo la Oyterbay Jijini humo ambalo litaonesha magari mapya, matoleo mapya ya pikipiki pamoja na burudani za kusisimua kwa ajili ya familia.

“Kwa mara ya kumi tunaandaa tamasha hili linaloshirikisha wadau mbalimbali wanaohusika na vyombo vya moto lengo letu likiwa ni kuendelea kuleta aina mbalimbali ya bidhaa za vyombo vya moto ili watumiaji wapate fursa ya kujifunza kuhusu bidhaa hizo,” alisema Nchahaga.

Nchahaga amevitaja baadhi ya vyombo vya moto na huduma shirikishi zitakazokuwepo kwenye maonesho hayo kuwa ni magari ya abiria na biashara, pikipiki, bodi za magari, sehemu za magari, mashine na zana zinazohusiana na magari.

Kwa upande wake Meneja Masoko wa Kampuni ya Bima ya Britam Insuarance, Oscar Ruhasha amesema kuwa Watanzania wengi hawana elimu juu ya bima hivyo kuwepo katika maonesho hayo kutawapa fursa ya kutoa elimu hiyo.

“Kwa sasa nchi imeendelea kwa kuwa na bima za aina nyingi hivyo ni muhimu kwa wananchi kupata elimu ya bima ili kuweza kufahamu bima ipi bora kwa matumizi husika,” alisema Ruhasha.

Tamasha hilo linalofanyika kila mwaka limeanzishwa mwaka 2008 ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘madereva kutoa fursa kwa madereva wenzao hata kama una haki’. Limedhaminiwa na Kampuni za Britam Insuarance, Zantel, CFAO Motors, Hyundai Motors, Insuarance, Lake Oil, Kiwango Security, Tindwa Medical, Automart, Coca Cola na Ipsos.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi