Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Mwakyembe Akabidhiwa Rasimu ya Katiba Mchezo wa Ngumi
Feb 04, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_28470" align="aligncenter" width="1000"] Mwenyekiti wa Kamati ya Kuandaa rasimu ya Katiba ya kusimamia mchezo wa Ngumi nchini Bw .Emmanuel Salehe akikabidhi rasimu ya katiba hiyo kwa Mheshimiwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe jana jijini Dar es Salaam katikati ni Katibu Mtendaji Baraza la Michezo la Taifa Bw. Mohamed Kiganja (Picha na Anitha Jonas).[/caption]

Na Anitha Jonas – WHUSM

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ameipongeza Kamati iliyoandaa rasimu ya katiba ya mchezo wa ngumi nchini kwa kumaliza kazi hiyo kwa wakati.

Mheshimiwa Mwakyembe ametoa kauli hiyo alipokuwa akikabidhiwa rasimu ya katiba hiyo jana jijini Dar es Salaam mara baada kukamilika kwa kuandaliwa kwake na kamati maalum iliyokuwa na wajumbe 13 wa kuteuliwa ambao walifanya kazi ya kuzunguka kwa wadau wa ngumi na kukusanya maoni.

“Nitateuwa watu saba kutoka katika kamati hii iliyounda rasimu watakao ungana na Baraza la Michezo la Taifa kuboresha rasimu hii ili tuweze kuitisha kikao kikubwa cha wadau wote wa mchezo wa ngumi na tuweze kuipitisha rasimu hii,”Dkt.Mwakyembe.

[caption id="attachment_28471" align="aligncenter" width="1000"] Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akizungumza na wadau wa ngumi (hawapo pichani) kuhusu mchakato wa kukamilisha rasimu ya katiba ya kusimamia mchezo wa ngumi nchini maara baada ya kukabidhiwa jana jijini Dar es Salaam,kulia kwake ni Msajili wa Vyama vya Michezo Nchini kutoka Baraza la Michezo la Taifa Bw. Ibrahim Mkwawa (Picha na Anitha Jonas)[/caption]

Akiendelea kuzungumza katika makabidhiano hayo Waziri Mwakyembe alieleza kuwa ataendelea kupokea maoni ya wadau hao ndani ya miezi mitatu kwa kuzingatia sheria ili kufanikisha kikao cha kupitisha rasimu hiyo ambacho kitaitishwa kwa mujibu wa sheria ili kufanikisha lengo la kuboresha sekta ya mchezo wa ngumi nchini.

Pamoja na hayo waziri huyo alisisitiza kuwa mapema wiki ijayo atamuagiza Katibu Mtendaji Baraza la Michezo la Taifa Bw. Mohamed Kiganja kutangaza wajumbe atakao kuwa amewateuwa kuungana na BMT katika kuboresha rasimu hiyo.

Akizungumza katika sherehe za makabidhiano ya rasimu hiyo ya katiba ya kusimamia mchezo wa ngumi nchini Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bw. Emmanuel Salehe alieleza kuwa pamoja na kukamilisha rasimu hiyo kamati hiyo iliunda pia kanuni za kusimamia mchezo wa ngumi kwa lengo la kuhakikisha misingi imara inawekwa katika kuboresha sekta ya mchezo huo.

[caption id="attachment_28472" align="aligncenter" width="1000"] Katibu Mtendaji Baraza la Michezo la Taifa Bw. Mohamed Kiganja (kulia) akitoa taarifa kuhusu mchakato wa kuundwa kwa rasimu ya katiba ya mchezo wa ngumi kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) kabla ya makabidhiano ya rasimu hiyo jana jijini Dar es Salaam,wapili kulia ni Msajili wa Vyama vya Michezo Nchini kutoka Baraza la Michezo la Taifa Bw Ibrahim Mkwawa (Picha na Anitha Jonas).[/caption]

Kwa Upande wa Katibu Mtendaji Baraza la Michezo la Taifa Bw. Mohamed Kiganja alisema kuwa ofisi yake iko tayari kuungana na wajumbe watakaoteuliwa na Mheshimiwa Waziri kukamilisha mchakato wa kuboresha rasimu hiyo kabla ya kupitishwa.

Pamoja na hayo naye bondia wa zamani aliyekwisha kushinda katika mikanda ya kimataifa Bw. Rashid Matumla alitoa maoni yake pamoja na kuipongeza Serikali kwa kufanya maamuzi ya kuundachombo imara kitakacho simamia mchezo wa ngumi kwa kuzingatia sheria tofauti na awali huku akiwasihi wadau wa ngumi kuacha tofauti zao na kuangalia suala la msingi kuboresha mazingira ya mchezo huo na kuufanya uwe na tija kwa zaidi pamoja na kuondoa mazingira yenye utata katika uendeshaji wa mchezo huo.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi