Waziri Mkuu Majaliwa Azindua Filamu ya ‘Tanzania Royal Tour’ Dodoma
May 15, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea zawadi kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka kwenye uzinduzi wa filamu ya ‘The Tanzania Royal Tour’ uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma Mei 15, 2022.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi walioshiriki katika uzinduzi wa filamu ya ‘The Tanzania Royal Tour’ katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma, Mei 15, 2022. Kutoka kushoto ni Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Pindi Chana, Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbas, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka, Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda na Spika wa Bunge Mstaafu, Anne Makinda.