Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Mkuu Awataka Viongozi wa UCSAF Kubaini Maeneo Yenye Changamoto za Mawasiliano Nchini.
Apr 30, 2019
Na Msemaji Mkuu

    [caption id="attachment_42596" align="aligncenter" width="800"] Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akipata maelezo juu ya huduma zinazotolewa na Shirika la Mawasiliano Nchini (TTCL) wakati wa maadhimisho miaka kumi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.[/caption]

Na Beatrice Lyimo -MAELEZO

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Mhe. Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa “Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote” kuendelea kubaini maeneo ambayo bado yana changamoto za mawasiliano nchini, ili Serikali iweze kupeleka huduma hiyo kwa walengwa mapema iwezekanavyo kabla ya 2020.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati wa Maadhimisho ya Miaka Kumi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UNCSFA), ikiwa ni lengo la kuhakikisha huduma za mawasiliano nchiini  zinakuwa bora na zenye kukidhi viwango endelevu, zenye tija na za uhakika.

[caption id="attachment_42609" align="aligncenter" width="800"] Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akihutubia wakati wa kuadhimisha miaka kumi ya mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.[/caption]

“Mfuko uendelee kufuatilia kwa karibu sehemu zilizojengwa minara ya mawasiliano kwa kutumia ruzuku ya serikali ili kuhakikisha wananchi katika maeneo hayo wanaendelea kunufaika na upatikanaji wa huduma bora za mawasiliano” ameeleza Waziri Mkuu, Majaliwa.

[caption id="attachment_42598" align="aligncenter" width="800"] Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akieleza mafanikio mbalimbali ya Mfuko wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) nchini ikiwemo kufanikisha huduma ya Mawasiliano nchini.[/caption]

Aidha amewataka Wananchi wote nchini kuendelea kuwa walinzi wa miundombinu ya mawasiliano, ikiwemo minara iliyojengwa katika maeneo yao ili waendelee kunufaika na uwekezaji uliofanywa na serikali.

[caption id="attachment_42600" align="aligncenter" width="800"] Naibu Waziri wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akizungumza wakati wa kuadhimisha miaka kumi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.Shonza amesema kuwa kwa kushirikiana na Mfuko huo wameweza kuboresha suala la usikivu wa Redio na Luninga nchini.[/caption]

“Watanzania tuendelee kutumia vizuri fursa ya mawasiliano kwa kutumia vyema mitandao ya simu kwa mawasiliano yenye tija, kuleta maendeleo na mshikamano baina yetu”

“Serikali itaendelea kupeleka mawasiliano katika sehemu zilizobaki hapa nchini ili wananchi waweze kunufaika na uwepo wa mawasiliano”. ameongeza Waziri Mkuu.

[caption id="attachment_42599" align="aligncenter" width="800"] Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) Mhandisi Peter Ulanga akieleza majukumu mbalimbali ya mfuko huo wakati wa kuadhimisha miaka kumi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.[/caption]

Aidha amesema kuwa, pamekuwapo na mafanikio mbalimbali ya Mfuko huo, ikiwemo kupeleka mawasiliano katika Kata 703, zenye vijiji 2,501 na wakazi zaidi ya milioni 5, pia imechangia shilingi bilioni 118 katika kuhakikisha huduma za mawasiliano zinawafikia wananchi.

[caption id="attachment_42601" align="aligncenter" width="800"] Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Dkt.Jim Yonaz akiwa na wageni mbalimbali wakati wa kuadhimisha miaka kumi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.[/caption]

Kwa upande wake Naibu Waziri (Sekta ya Mawasiliano) Mhandisi Atashasta Nditiye amesema kuwa UCSAF ilianzishwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Sheria ya Bunge namba 11 ya mwaka 2006, kwa lengo la kupeleka na kufanikisha huduma ya mawasiliano kwa wananchi waishio katika maeneo machache ya mijini na maeneo yaliyo mbali vijijini yasiyo na mvuto wa kibiashara kwa watoa huduma ya mawasiliano.

[caption id="attachment_42597" align="aligncenter" width="800"] Bango la Umoja wa Wamachinga Jiji la Dodoma wakimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kwa kuwatambua wajasiriamali wadogo wadogo leo wakati wa kuadhimisha miaka kumi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.[/caption]

“Kuna Mafanikio mbalimbali ya Mfuko ikiwemo utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2015 la kufanikisha huduma ya Mawasiliano nchini|”ameongeza Mhandisi Nditiye.

Nae, Mtendaji Mkuu Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote Mhandisi Peter Ulanga amebainisha kuwa ili kuweza kufikia Malengo Mfuko una Majukumu mbalimbali ikiwemo kuweka vigezo vya utambuzi na maeneo ya vijiji vinavyohitaji na ambavyo haviwezi kupata huduma ya mawasiliano kwa sababu havina mvuto wa kibiashara.

[caption id="attachment_42606" align="aligncenter" width="800"] Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akisalimiana na mmoja wa watumishi wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) wakati wa maadhimisho miaka kumi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.[/caption]

“Pia jukumu jingine la Mfuko ni kubaini maeneo ya miradi ya mawasiliano ambayo yanaweza kuoata ruzuku kutoka katika Mfuko na kuangalia njia sahihi za kutoa ruzuku kwa ajili ya kupeleka huduma ya mawasiliano vijijini na katika maeneo yasiyo na mvuto kibiashara” ameongeza Mhandisi Ulanga.

Mbali na hayo, Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) unatekeleza miradi mbalimbali ikiwemo Mradi wa kuunganisha shule kwa intaneti, mradi wa Tiba Mtandao, Mradi wa matangazo ya kidigitali ya runinga, I-knowledge na mafunzo ya TEHAMA kwa walimu.

     

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi