[caption id="attachment_36622" align="aligncenter" width="750"] Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwahutubia wananchi wa Kibakwe wilayani Mpwampwa, akiwa kwenye ziara mkoani Dodoma, Oktoba 10, 2018.[/caption]
WAZIRI MKUU Kassim ametoa siku 10 kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa, Bw. Peter Swea awe ametoa fedha za mikopo kwa ajili ya vijana, wanawake na walemavu.
"Leo ni tarahe 10 nataka hadi ikifika tarehe 20 ya mwezi huu uwe umeshatoa fedha za mikopo kwa wanawake, vijana na walemavu. Habari za mpaka kikao kiridhie hayo ni mambo ya zamani na ndio maana ikatungwa sheria kwa ajili ya jambo hilo. "
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Oktoba 10, 2018) wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Kibakwe wilayani Mpwapwa mara baada ya kukagua ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kibakwe, akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Dodoma.
[caption id="attachment_36619" align="aligncenter" width="750"] Mke wa Waziri Mkuu Marry Majaliwa, akiwasalimia wananchi wa Kata ya Kibakwe wilayani Mpwampwa mkoani Dodoma, Oktoba 10, 2018.[/caption]Waziri Mkuu ametoa agizo hilo baada ya Mkurugenzi huyo kumueleza kuwa bado hajatoa fedha kwa ajili ya mikopo hiyo ambazo alipaswa kuzitoa kila robo mwaka, akidai bado kikao cha kuidhinisha hakijakaa.
Amesema fedha hizo ambazo ni asilimia 10 ya mapato ya ndani yanayokusanywa kwenye halmashauri, ambapo anatakiwa kutumia asilimia nne kwa ajili ya mikopo ya wanawake, asilimia mikopo kwa ajili ya vijana na asilimia mbili zitolewe kwa walemavu.
Kadhalika,Waziri Mkuu amewaagiza watendaji wote wa vijiji kuainisha maeneo yote yenye misitu na vyanzo vya maji pamoja na kuwachukulia hatua kali watu wote watakaobainika kukata miti bila kibali.
[caption id="attachment_36618" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Binilith Mahenge, akizungumza na wananchi wa Kibakwe wilayani Mpwampwa, kwenye ziara ya Waziri Mkuu mkoani Dodoma, Oktoba 10, 2018.[/caption]Amesema mtu yeyote atakayebainika kukata miti bila kibali achukuliwe hatua kali kwa sababu wamekuwa wakisababisha ukosefu wa maji, ambapo wakandarasi wa maji kwenye wilaya hiyo wanapata changamoto ya kukosa maji kwenye maeneo mengo wakati awali Mpwapwa awali ilikuwa na ardhi ya chepechepe.
"Nimepata habari, hapa Kibakwe watu wanakata miti ili kushindana ubavu wao wa kuishi. Nawaagiza watendaji wote wa vijiji kuainisha maeneo yenye vyanzo vya maji na misitu na muyalinde. Madiwani pia mnatakiwa kushiriki kukemea ukataji miti.”
[caption id="attachment_36620" align="aligncenter" width="750"] Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Mbunge wa Mpwapwa George Lubeleje, baada ya kukagua ujenzi wa kituo cha afya Kibakwe Wilayani Mpwapwa, akiwa kwenye ziara ya mkoa Dodoma, Oktoba 10, 2018[/caption]Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Bw. Jabir Shekimweli ameishukuru Serikali kwa kutenga sh. bilioni 1.4 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa vituo vitatu vya afya ambavyo ni Kibakwe, Mima na Pwaga.
Amesema miradi hiyo imesimamiwa vizuri na kamati za ujenzi kwenye kata na vijiji husika kama ambavyo muongozo ulivyoelekeza.
[caption id="attachment_36617" align="aligncenter" width="750"] Wananchi wa Kata ya Kibakwe wilayani Mpwampwa wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakati akiwahutubia wananchi hao, akiwa kwenye ziara mkoani Dodoma, Oktoba 10, 2018.[/caption]Nae Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, Bw. George Simbachawene amesema utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) umefanyika kwa mafanikio makubwa kwenye sekta ya afya, umeme na elimu.
Mbunge huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, ameomba ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kutoka Kongwa, Mpwapwa hadi Kibakwe, uharakishwe ili kuondoa adha ya miundombinu inayowakabili wananchi.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
41193 – Dodoma
JUMATANO, OKTOBA 10, 2018.