Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Mkuu Atembelea Mradi wa Kuzalisha Umeme Kijiji cha Mahumbika
Jul 14, 2017
Na Msemaji Mkuu

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, akipokea maelezo ya mradi wa kuzalisha umeme unaojengwa katika kijiji cha Mahumbika wilayani Lindi kutoka kwa Mhandisi Jafary Msuya, wakati alipotembelea mradi huo. Waziri Mkuu yupo Mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya siku nne. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, akipokea maelezo ya mradi wa kuzalisha umeme unaojengwa katika kijiji cha Mahumbika wilayani Lindi kutoka kwa Mhandisi Ferdinand Mwinje, wakati akikagua mradi huo. Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Prof. James Mdoe, wakati alipotembelea mradi wa kuzalisha umeme unaojengwa katika kijiji cha Mahumbika wilayani Lindi. Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne (katikati) ni Mbunge wa Jimbo la Mtama Nape Mnauye. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiongea na wananchi, wakati alipotembelea mradi wa kuzalisha umeme wa Mahumbika, unaojengwa katika kijiji cha Mahumbika wilayani Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)​

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi