Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya Shilingi milioni 200 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi, ambao ni mchango uliotolewa na Benki hiyo kwa ajili ya upimaji na matibabu ya saratani ya shingo ya uzazi kwa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, kwenye mbio za NBC Dodoma Marathon zilizofanyika jijini Dodoma. Julai 31, 2022.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikabidhi hundi ya Shilingi milioni 200, kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dkt. Julius Mwaiselage, ambao ni mchango uliyotolewa na Benki hiyo kwa ajili ya upimaji na matibabu ya saratani ya shingo ya uzazi kwa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, kwenye mbio za NBC Dodoma Marathon zilizofanyika jijini Dodoma. Julai 31, 2022.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati aliposhiriki katika mbio za NBC Dodoma Marathon zilizofanyika jijini Dodoma. Julai 31, 2022.